Home Sports KOCHA MAKI WA SIMBA ALIA NA RATIBA KUBANA

KOCHA MAKI WA SIMBA ALIA NA RATIBA KUBANA

KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Maki amesema kuwa alipata muda mdogo kufanya maandalizi kuikabili Geita Gold kutokana na kumaliza mchezo dhidi ya Yanga wa Ngao ya Jamii,Uwanja wa Mkapa.

 Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 huku mabao ya Yanga yakifungwa na Fiston Mayele ambaye alifunga mabao yote mawili na lile la Simba likifungwa na Pape Sakho.

 Maki amesema kuwa walipata muda mdogo kufanya mandalizi Kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Geita Gold.

“Jumamosi tulikuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga,Jumapili,Jumatatu na Jummane hizi ni siku ambazo tulipaswa kufanya maandalizi lakini huwezi kufanya maandalizi ndani ya siku mbili hii ni ngumu kwetu.

“Lakini wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo tutapambana ili kuweza kufanya kazi yetu ya kusaka ushindi na kisaikolojia tumewaandaa ili waweze kuwa katika ari ya kusaka ushindi,” amesema Maki.

Jana Simba walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo na miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi ni pamoja na kiungo Sadio Kanoute, beki Joash Onyango na Mohamed Hussein.

 Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kwa msimu wa 2022/23 na wataanzia nyumbani tofauti na msimu wa 2021/22 walipoanzia ugenini mbele ya Biashara United na waliweza kugawana pointi mojamoja.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Karume, Mara ambapo John Bocco aliweza kukosa penalti kwenye mchezo huo.

Previous articleHII HAPA RATIBA YA LIGI LEO NA MATOKEO
Next articleKIUNGO SERGIO GOMEZ NI MALI YA CITY