Home International KIUNGO SERGIO GOMEZ NI MALI YA CITY

KIUNGO SERGIO GOMEZ NI MALI YA CITY

SERGIO Gomez ambaye ni kiungo amesaini dili la miaka minne kuweza kuitumikia Klabu ya Manchester City.

City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England wameinasa saini ya nyota huyo ili aweze kupata changamoto mpya ndani ya Ligi Kuu England.

Nyota huyo mwenye miaka 21 amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 11 akitokea Klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Gomez ni usajili wa nne wa Kocha Mkuu, Pep Guardiola ambaye anakiongoza kikosi hicho kuweza kutetea taji la ligi kwa mara nyingine kwa msimu wa 2022/23.

Wengine ambao wamesajiliwa hapo ni pamoja na Erling Haaland,Kalvin Phillips na Stefan Ortega.

Previous articleKOCHA MAKI WA SIMBA ALIA NA RATIBA KUBANA
Next articleMSAKO WA POINTI TATU ZA YANGA MBELE YA POLISI TANZANIA