Home Sports YANGA KAZINI LEO KUIVAA POLISI TANZANIA

YANGA KAZINI LEO KUIVAA POLISI TANZANIA

BAADA ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba,Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi leo Agosti 16 inafungua ukurasa kwenye Ligi Kuu Bara kwa kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania.

Yanga waliweza kutetea taji lao la kwanza ambalo walitwaa msimu uliopita wa 2021/22 ambapo walitwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Mtupiaji kwa msimu wa 2021/22 alikuwa ni Fiston Mayele ambaye msimu huu wa 2022/23 amewatungua kwa mara nyingine Simba Uwanja wa Mkapa mabao yote mawili na kuipa taji la kwanza Yanga.

Nabi ameweka wazi kwamba anatambua mchezo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kuweza kupata matokeo.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji kupata pointi tatu muhimu,timu ambayo tunakutana nayo ni imara hivyo nasi tuna kazi ya kufanya hilo lipo wazi”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo na timu Arusha ni pamoja na Fiston Mayele,Bernard Morrison,Aziz KI na Aboutwalib Mshery.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo majira ya 10:00 jioni.

Previous articleSHINDA VIBUNDA KUPITIA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET
Next articleMAKI KWENYE KIBARUA KINGINE