Home Sports KOCHA MAKI ATAJA KILICHOSABABISHA KUFUNGWA NA YANGA

KOCHA MAKI ATAJA KILICHOSABABISHA KUFUNGWA NA YANGA

ZORAN Maki, Kocha Mkuu wa Simba amesema walikosa umakini kipindi cha pili jambo lililowafanya wakafungwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Baada ya dk 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-1 Simba.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele dk ya 49 na 80 lilikuwa ni bao la ushindi kwenye mchezo huo baada ya kumtungua Beno Kakolanya.

Bao la Simba lilifungwa na Pape Sakho ambaye aliweza kupachika bao hilo akitumia pasi ya Clatous Chama.

Maki amesema:”Ilikuwa ni mechi ngumu na yenye ushindani mkubwa tulishindwa kwenye umakini katika kipindi cha kwanza jambo ambalo lilitufanya tushindwe kufanya vizuri,”.

Previous articleJINA LA MESSI HALIPO KWENYE TUZO YA BALLON D’OR
Next articleVIDEO:NABI:DABI ILIKUWA YAKIMBINU,TULIWAPA KUJIAMINI KUCHEZA