Home International JINA LA MESSI HALIPO KWENYE TUZO YA BALLON D’OR

JINA LA MESSI HALIPO KWENYE TUZO YA BALLON D’OR

JINA la Lionel Messi halijatajwa kwenye tuzo ya kuwania katika orodha ya wachezaji 30 ambao wanawania Tuzo ya Ballond’Or.

Messi ambaye ana rekodi ya kubeba tuzo hiyo mara saba zikiwa ni nyingi kushinda wachezaji wengine hayupo kwenye orodha iliyotolewa Ijumaa.

Sherehe za tuzo hiyo znatarajiwa kufanyika Oktoba 17 mwaka huu Paris,Ufaransa.

Kwenye orodha hiyo,Messi anayecheza PSG amekosekana pia staa mwenzake Neymar raia wa Brazil lakini mpinzani wake Cristian Ronaldo jina lake lipo yeye anacheza Manchester United.

Jina la Karim Benzema linatajwa kupewa chapuo ya kuweza kutwaa tuzo hiyo yeye anacheza Real Madrid.

Pia mwingine ambaye yupo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mohamed Salah wa Liverpool na Sadio Mane wa Bayern Munich.

Previous articleVIDEO:SIMBA WAMKATAA MZUNGU WAO
Next articleKOCHA MAKI ATAJA KILICHOSABABISHA KUFUNGWA NA YANGA