Home Sports YANGA WAPINDUA MEZA MBELE YA POLISI TANZANIA

YANGA WAPINDUA MEZA MBELE YA POLISI TANZANIA

 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamefungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.

Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kasi mwanzomwisho, mabao yalifungwa na Salum Kipemba dk ya 34 kwa Polisi Tanzania yale ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele dk ya 41 na Bakari Mwamnyeto dk ya 85.

Mayele aliweza kukosa penalti kwenye mchezo huo dk ya 11 baada ya pigo hilo kuweza kuokolewa na mlinda mlango wa Polisi Tanzania.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi licha ya kupata ushindi mwishoni malengo yao yamemefanikiwa.

“Ilikuwa ni mechi ngumu lakini tumeweza kupata ushindi hilo ni jambo la muhimu kwetu hivyo tunaendelea kusaka ushindi kwa mechi zijazo,” amesema.

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA POLISI TANZANIA
Next articleSAUTI:MZUNGU WA SIMBA ANA KAZI NZITO YA KUFANYA