SAIDO: SIKUTAKA KUONDOKA YANGA
MARA baada ya Yanga kutangaza kuachana rasmi na Said Ntibazonkiza ‘Saido’, mashabiki na wadau wengi wa soka walishitushwa na taarifa hiyo wengine hawakuamini kabisa kilichotokea. Hii inatokana na jinsi gani Saido alikuwa na mchongo mkubwa ndani ya timu hii ndio iliwafanya watu wawe wagumu kuamini. Mashabiki wa Yanga na wengine ambao sio wa timu hiyo…
WAKALI WA KUTUPIA BONGO
NDANI ya Ligi Kuu Bara kuna wakali wa kucheka na nyavu ambao wanatimiza majukumu yao katika timu zao. Ni George Mpole mali ya Geita Gold huyu ni mzawa mwenye mabao mengi kwa msimu huu akiwa ametoa pia pasi tatu za mabao. Mpole kahusika kwenye mabao 17 kati ya 26 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayonolewa…
PLATIN NA BLATTER KESI YAO INAUNGURUMA
SEPP Blatter na Michel Platin ni majina makubwa katika soka ambao kwa pamoja leo wanaingia mahakamani kuendelea kujibu mashtaka ya kujihusisha na rushwa enzi za utawala wao. Blatter na Platin wanashitakiwa kwa kosa la kuhamisha zaidi ya kiasi cha Euro milioni 1.6 mwaka 2011 kinyume na utaratibu kutoka akaunti ya benki ya Blatter kwenda Platin…
MANCHESTER CITY WAMTAKA SAKA
IMEELEZWA kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City wanahitaji saini ya staa wa Arsenal, Bukayo Saka katka kipindi cha miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake. City wanahitaji kumpata nyota huyo ili aweze kuondoka ndani ya kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta. Inaelezwa kuwa City pamoja na wapinzani wao wakubwa Liverpool…
YANGA YAPIGA 8-0 FRIENDS RANGERS
KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi jana kiliibuka na ushindi wa mabao 8-0 Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki. Mabao ya Yanga yalifungwa na kiungo Dennis Nkane ambaye alitupia kamba mbili, Fiston Mayele alitupia kambani mara moja mzee wa kuwajaza Heritier Makambo yeye alitupia kamba mbili. Mshambuliaji chipukizi wa timu hiyo Yusuph…
POULSEN:ALGERIA NI WAGUMU ILA TUTAPAMBANA
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wataingia kwa kuwaheshimu wapinzani wao Algeria kwa kuwa ni timu imara na ina uzoefu mkubwa. Poulsen amebanisha kuwa kwa ubora walionao Algeria ni wazi Tanzania inatakiwa kuingia uwanjani ikiwa na mpango maalum kwa kuwa timu hiyo ni imara kwenye umiliki wa mpira….
SENZO ATAJA SABABU ZA KUKUSANYA BILIONI YANGA
MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza amesema kupitia mfumo wa kidigitali wa mabadiliko ya Klabu ya Yanga ulioasisiwa mapema mwaka huu klabu hiyo imeingiza zaidi ya Bilioni moja za kitanzania. Senzo amebainisha kuwa kwa msimu wa mwaka 2019 Yanga ilikusanya zaidi ya kiasi cha milioni 9 kupitia pesa za usajili wa wanachama,…
SIMBA WATAJA SIKU YA KUMTANGAZA KOCHA MPYA
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatarajia kumaliza mchakato wa kupitia maombi na kumchagua kocha mpya wa kikosi hicho katika kipindi cha wiki mbili ambazo ni sawa na siku 14. Simba Mei 31, mwaka huu walitangaza rasmi kufikia makubaliano ya kuachana na kocha wao, Pablo Franco na kocha wa viungo, Daniel Castro, kwa kile kilichoelezwa…
KUNA MKATABA WA STRAIKA MZAMBIA UMENASWA NA GSM
KUNA mkataba wa staraika Mzambia umenaswa na GSM ni ndani ya gazeti la Championi Jumatano
SURE BOY:NILITAMBUA NITAKUTA USHINDANI WA NAMBA YANGA
KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amekiri kukutana na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi hicho, lakini kamwe hatakubali kukaa benchi na badala yake atapambania nafasi yake. Staa huyo amekutana na ushindani wa namba wa viungo kutoka kwa Mganda, Khalid Aucho, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Yannick Bangala na Zawadi Mauya. Sure Boy…
VIDEO:CHEKI MAZOEZI YA STARS KUIKABILI ALGERIA
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Juni 7 wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuikabili Algeria kesho, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
TAIFA STARS KAMILI,HIMID MAO KUKOSEKANA KESHO
KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania wapo tayari kuelekea mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON. Mchezo huo utakuwa ni dhidi ya Algeria utakaochezwa kesho Juni 8, 2022 saa 1:00 usiku huku akiweka wazi kwamba wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu. Poulsen…
SERENGETI GIRLS YATINGA BUNGENI
LEO Juni 7,2022,Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana U17 Serengeti Girls wameweza kuingia kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Serengeti Girls wamealikwa bungeni baada ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia litakalofanyika India mwaka huu kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-1 Cameroon. Kete ya kwanza walianza ugenini ambapo waliweza kushinda…
YANGA YAKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA WANACHAMA
MKURUGENZI Mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh amesema ndani ya miezi 6 wameweza kusajili wanachama 34,650. Huu ulikuwa ni mchakato wa Klabu ya Yanga kuweza kufanya usajili kwa wanachama baada ya kubadili katiba na mfumo wa uendeshaji wa timu. Akizungumza leo Juni 7, Saleh amesema kuwa wameweza kukusanya fedha hizo ikiwa ni mafanikio makubwa ndani ya miezi…
MODRIC NDOTO ZAKE ZILITIMIA
KIUNGO wa Real Madrid, Luka Modric ameweka wazi kuwa ndoto zake zilitimia baada ya kusajiliwa ndani ya kikosi hicho. Madrid ilimsajili Modric 2012 akitokea Klabu ya Tottenham na yupo Madrid kwa miaka 10 sasa. Kiungo huyo mwenye miaka 36 amezidi kuwa bora licha ya umri ambao anao kwa sasa ambao unaonekana kumtupa mkono na mwaka…
AZAM FC WAJA NA MIPANGO MIPYA
UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa msimu ujao utafanya vizuri kwa kutumia makosa ambayo wameyafanya msimu huu. Ikiwa imecheza mechi 26 kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 na imekusanya pointi 37 kibindoni huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 64. Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwa namna ambavyo wanakwenda…