Home Uncategorized SENZO ATAJA SABABU ZA KUKUSANYA BILIONI YANGA

SENZO ATAJA SABABU ZA KUKUSANYA BILIONI YANGA

 MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza amesema kupitia mfumo wa kidigitali wa mabadiliko ya Klabu ya Yanga ulioasisiwa mapema mwaka huu klabu hiyo imeingiza zaidi ya Bilioni moja za kitanzania.

Senzo amebainisha kuwa kwa msimu wa mwaka 2019 Yanga ilikusanya zaidi ya kiasi cha milioni 9 kupitia pesa za usajili wa wanachama, msimu wa 2020 Yanga ilikusanya kiasi cha milioni 6.5 na msimu uliopita Yanga ilikusanya zaidi ya milioni 21 kupitia usajili wa wanachama.

“Kwenye kikao chetu na Makamu Mwenyekiti alisema watu hawawezi kuamini kama tukiwaambia kuhusu namba hizi lakini tumekusanya zaidi ya bilioni moja kwa kipindi cha miezi sita tu.

“Kumekuwa na changamoto ambazo tunazifanyia kazi kwa kushirikiana na Kampuni ya Kili net kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha zoezi hili kwenda vizuri kwa kipindi cha miezi sita tangu mradi ulipoanza.

“Bado tunaendelea kufanya hili zoezi kwa wanachama wote na tunaomba waendelee kuwa nasi kwa kuwa haya yanatokea baada ya kuweza kufanya mabadiliko ya katiba na sasa tupo kwenye mwendo,” amesema.

Previous articleSIMBA WATAJA SIKU YA KUMTANGAZA KOCHA MPYA
Next articlePOULSEN:ALGERIA NI WAGUMU ILA TUTAPAMBANA