Home Sports POULSEN:ALGERIA NI WAGUMU ILA TUTAPAMBANA

POULSEN:ALGERIA NI WAGUMU ILA TUTAPAMBANA

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wataingia kwa kuwaheshimu wapinzani wao Algeria kwa kuwa ni timu imara na ina uzoefu mkubwa.

Poulsen amebanisha kuwa kwa ubora walionao Algeria ni wazi Tanzania inatakiwa kuingia uwanjani ikiwa na mpango maalum kwa kuwa timu hiyo ni imara kwenye umiliki wa mpira.

“Ni mchezo mgumu na unaweza kuniuliza kwamba namna gani tunaweza kuwazuia Algeria? Hilo lipo wazi kwa kuwa presha haiwezi kukosekana hasa unapocheza na timu imara na kubwa kwenye mashindano haya makubwa.

“Tuna wachezaji wazuri ambao wapo kwenye timu na wanafanya vizuri hata wanapoanzia benchi haya ni matokeo mazuri kushindwa kwetu kushinda mbele ya Niger ni somo kwetu licha ya kwamba tulipata bao la mapema.

“Ambacho kiliweza kutokea ninaweza kusema kwamba tulifungwa bao jepesi kutokana na makosa ya mawasiliano kati ya beki na mlinzi hivyo ni sehemu ya kufanyia kazi makosa yetu,”.

Taifa Stars inawakaribisha Algeria kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa pili wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Kiungo Himi Mao kwa mujibu wa Poulsen anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kutokana na kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Niger,Benin.

Previous articleSENZO ATAJA SABABU ZA KUKUSANYA BILIONI YANGA
Next articleYANGA YAPIGA 8-0 FRIENDS RANGERS