Home Uncategorized SIMBA WATAJA SIKU YA KUMTANGAZA KOCHA MPYA

SIMBA WATAJA SIKU YA KUMTANGAZA KOCHA MPYA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatarajia kumaliza mchakato wa kupitia maombi na kumchagua kocha mpya wa kikosi hicho katika kipindi cha wiki mbili ambazo ni sawa na siku 14.

Simba Mei 31, mwaka huu walitangaza rasmi kufikia makubaliano ya kuachana na kocha wao, Pablo Franco na kocha wa viungo, Daniel Castro, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho.

Taarifa hiyo pia iliweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola mpaka mwisho wa msimu.

Mchezo wa mwisho kwa Pablo kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Yanga ambapo alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 ilikuwa hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema: “Tangu tulipotangaza kuachana na aliyekuwa kocha wetu mkuu, Pablo Franco tumekuwa tunapokea wasifu (CV) za makocha mbalimbali kutokea nchi nyingi duniani ambao wanaonyesha nia ya kuhitaji nafasi ya kufundisha Simba.

“Tunatarajia kukamilisha mchakato huu wa kutafuta kocha mpya katika kipindi cha wiki mbili, ni mapema kwa sababu tunataka kocha mpya apate nafasi ya kufanya tathmini ya kikosi chake na kujua ni wapi anapoona mapungufu na anahitaji parekebishwe.

Previous articleKUNA MKATABA WA STRAIKA MZAMBIA UMENASWA NA GSM
Next articleSENZO ATAJA SABABU ZA KUKUSANYA BILIONI YANGA