Home Sports TAIFA STARS KAMILI,HIMID MAO KUKOSEKANA KESHO

TAIFA STARS KAMILI,HIMID MAO KUKOSEKANA KESHO

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania wapo tayari kuelekea mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON.

Mchezo huo utakuwa ni dhidi ya Algeria utakaochezwa kesho Juni 8, 2022 saa 1:00 usiku huku akiweka wazi kwamba wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu.

Poulsen amesema:”Mchezo utakuwa mgumu hasa ukizingatia kwamba tunacheza na timu imara ambayo imetoka kucheza na Uganda na tuliangalia namna ambavyo waliweza kufanya vizuri.

“Kikubwa ni kwamba ushindani ambao upo na uimara wa timu ambayo tunakutana nayo inatufanya tuzidi kujua kwamba kazi haitakuwa nyepesi hasa uwezo wao katika umiliki.

“Unaweza ukajiuliza ni kwa namna gani tunaweza kuwazuia na kukabiliana na presha kwenye mchezo huo hilo lipo wazi lakini tutaingia uwanjani tukijiamini hasa kwa kuwa tupo nyumbani,” amesema Poulsen.

Mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuweza kuishangilia timu hiyo ambayo imetoka kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Niger kwenye mchezo uliochezwa Benin.

Kwa mujibu wa Poulsen ni Himid Mao ataukosa mchezo wa kesho kutokana na maumivu ambayo alipata kwenye mchezo dhidi ya Niger.

Previous articleSERENGETI GIRLS YATINGA BUNGENI
Next articleVIDEO:CHEKI MAZOEZI YA STARS KUIKABILI ALGERIA