Home Sports SERENGETI GIRLS YATINGA BUNGENI

SERENGETI GIRLS YATINGA BUNGENI

LEO Juni 7,2022,Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana U17 Serengeti Girls wameweza kuingia kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serengeti Girls wamealikwa bungeni baada ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia litakalofanyika India mwaka huu kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-1 Cameroon.

Kete ya kwanza walianza ugenini ambapo waliweza kushinda kwa mabao 4-1 kisha mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar waliweza kushinda kwa bao 1-0.

Nahodha wa Serengeti Girls,Noela Patrick alipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Wabunge ambapo aliweza kutoa shukrani kwa Serikali kuwa bega kwa bega na timu hiyo.

Previous articleYANGA YAKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA WANACHAMA
Next articleTAIFA STARS KAMILI,HIMID MAO KUKOSEKANA KESHO