Home Sports YANGA YAKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA WANACHAMA

YANGA YAKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA WANACHAMA

MKURUGENZI Mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh amesema ndani ya miezi 6 wameweza kusajili wanachama 34,650.

Huu ulikuwa ni mchakato wa Klabu ya Yanga kuweza kufanya usajili kwa wanachama baada ya kubadili katiba na mfumo wa uendeshaji wa timu.

Akizungumza leo Juni 7, Saleh amesema kuwa wameweza kukusanya fedha hizo ikiwa ni mafanikio makubwa ndani ya miezi 6.

“Ndani ya kipindi cha miezi 6 tumeweza kusajili wanachama 34,650 na kukusanya kukusanya bilioni 1.07.

“Bado kuna mpango mwingine wa kuweza kufanya maboresho kwenye usajili hivyo wanachama wazidi kuwa na subira mengi yanakuja,”.

Previous articleMODRIC NDOTO ZAKE ZILITIMIA
Next articleSERENGETI GIRLS YATINGA BUNGENI