Home Sports MODRIC NDOTO ZAKE ZILITIMIA

MODRIC NDOTO ZAKE ZILITIMIA

KIUNGO wa Real Madrid, Luka Modric ameweka wazi kuwa ndoto zake zilitimia baada ya kusajiliwa ndani ya kikosi hicho.

Madrid ilimsajili Modric 2012 akitokea Klabu ya Tottenham na yupo Madrid kwa miaka 10 sasa.

Kiungo huyo mwenye miaka 36 amezidi kuwa bora licha ya umri ambao anao kwa sasa ambao unaonekana kumtupa mkono na mwaka 2018 alitwaa tuzo ya Ballon d’Or.

Kiungo huyo amesema:”Ndoto zangu zote zimetimia baada ya kujiunga na Madrid. Matumaini yangu ni kuona nastaafu nikiwa hapa,”.

Previous articleAZAM FC WAJA NA MIPANGO MIPYA
Next articleYANGA YAKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA WANACHAMA