Home Sports AZAM FC WAJA NA MIPANGO MIPYA

AZAM FC WAJA NA MIPANGO MIPYA

 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa msimu ujao utafanya vizuri kwa kutumia makosa ambayo wameyafanya msimu huu.

Ikiwa imecheza mechi 26 kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 na imekusanya pointi 37 kibindoni huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 64.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwa namna ambavyo wanakwenda msimu huu haujawa mzuri kwao hivyo wanapambana kupata matokeo mazuri.

“Kwetu sisi haujawa msimu mzuri ukitazama namna ambavyo matokeo tunapata na hatujaependa kupata hiki hasa ukizingatia kwamba mashabiki wanapenda matokeo mazuri hata sisi tunapenda matokeo mazuri.

“Kumbuka kwamba ni timu kubwa ina wachezaji wakubwa ambao wamecheza kutoka timu  kubwa na wanachokipata hapa kwa upande wa matokeo hawapendezwi nacho hivyo tuna muda wa kujipanga upya kwa ajili ya wakati ujao,” amesema

Previous articleVIDEO:ALLY MAYAY,WAARABU NI WAJANJA AWACHAMBUA MPOLE NA MAYELE
Next articleMODRIC NDOTO ZAKE ZILITIMIA