Home Sports WAKALI WA KUTUPIA BONGO

WAKALI WA KUTUPIA BONGO

NDANI ya Ligi Kuu Bara kuna wakali wa kucheka na nyavu ambao wanatimiza majukumu yao katika timu zao.

Ni George Mpole mali ya Geita Gold huyu ni mzawa mwenye mabao mengi kwa msimu huu akiwa ametoa pia pasi tatu za mabao.

Mpole kahusika kwenye mabao 17 kati ya 26 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro.

Mwingine ni Fiston Mayele mzee wa kutetema huyu yupo zake ndani ya Yanga akiwa ametupia mabao 14 na ana pasi tatu pia za mabao.

Relliats Lusajo ana jambo ambalo limemkuta kwa kuwa alikuwa wa kwanza kufikisha mabao 10 ila bado kaganda hapo kwa muda akiwa ni namba moja ndani ya Namungo kwa washambuliaji wenye mabao mengi.

Rodgers Kola anakimbiza ndani ya Azam FC akiwa ametupia mabao 9 huku Meddie Kagere wa Simba akiwa ametupia mabao 7 kama Said Ntibanzokiza yule wa Yanga.

Previous articlePLATIN NA BLATTER KESI YAO INAUNGURUMA
Next articleSAIDO: SIKUTAKA KUONDOKA YANGA