Home Sports SURE BOY:NILITAMBUA NITAKUTA USHINDANI WA NAMBA YANGA

SURE BOY:NILITAMBUA NITAKUTA USHINDANI WA NAMBA YANGA

KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amekiri kukutana na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi hicho, lakini kamwe hatakubali kukaa benchi na badala yake atapambania nafasi yake.

Staa huyo amekutana na ushindani wa namba wa viungo kutoka kwa Mganda, Khalid Aucho, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Yannick Bangala na Zawadi Mauya.

Sure Boy amejiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Azam FC baada ya kuomba mkataba wake uvunjwe.

 Sure Boy amesema kabla ya kukubali kusaini Yanga, alifahamu ushindani atakaokwenda kukutana nao kutoka kwa viungo wa timu hiyo.

Sure Boy alisema kuwa, licha ya kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mtunisia, Nasreddine Nabi, lakini bado hajaridhika, hivyo amepanga kuendelea kuonesha kiwango bora ili aendelee kucheza.

Aliongeza kuwa, kikubwa alichopanga ni kuendelea kufanya mazoezi binafsi ili kufanikisha malengo yake ya kuendelea kucheza kwa kiwango kizuri.

Previous articleVIDEO:CHEKI MAZOEZI YA STARS KUIKABILI ALGERIA
Next articleKUNA MKATABA WA STRAIKA MZAMBIA UMENASWA NA GSM