
PRESHA YA SIMBA IPO KWENYE TIMU HII HAPA
KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Hitimana Thierry, amefunguka kuwa kasi waliyoanza nayo wapinzani wao, Yanga na mabao wanayofunga, imekuwa ikiwaongezea presha kubwa ya kuhakikisha wanapata matokeo katika mechi zao.Simba imepoteza pointi nne katika mechi tano ilizocheza, ikiwa imeshinda tatu na sare mbili. Ilianza kwa suluhu dhidi ya Biashara United kabla ya kuifunga Dodoma Jiji bao 1-0, kisha ikaifunga Polisi Tanzania bao 1-0, halafu ikasuluhu na Coastal Union kabla ya kuichapa Namungo…