Home International SALAH NI BORA DUNIANI

SALAH NI BORA DUNIANI

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Fernando Torres amesema kuwa nyota Mohamed Salah ambaye ni mshambuliaj ndiye mchezaji bora kwa sasa duniani.

 

Salah anawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya dunia ambayo itatolewa mwezi ujao na Shirikisho la Soka la Kimataifa,(Fifa) na watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa anastahili kutwaa tuzo hiyo.

Torres aliweza kuutazama mchezo wa Ligi ya Mabingwa wakati timu yake ya zamani ya Liverpool ilipokuwa ikicheza dhidi ya Atletico Madrid na aligushwa na kiwango cha nyota huyo raia wa Misri.

Amebainisha kuwa kwa sasa kwenye dunia hii huwezi kumfananisha Salah na mchezaji mwingine yule kutokana na ubora wake kwa asilimia 100 anaweza kuwa mchezaji bora zaidi.

“Kwa asilimia 100, naamini kuwa huyu ndiye mchezaji bora zaidi wa dunia kwa sasa, amekuwa na wakati mzuri sana kwenye kipindi hiki cha misimu miwili,”.

Previous articleISHU YA CHAMA KURUDI BONGO,YANGA,SIMBA ZATAJWA
Next articlePOULSEN AKUBALI UWEZO WA WACHEZAJI WAKE