GUARDIOLA AKUBALI MUZIKI WA UNITED

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amekubali muziki wa wapinzani wake Manchester United kwa kuweka wazi kuwa ina wachezaji wazuri.

Majira ya saa 9:30 muda wa kujipatia msosi Manchester United itakuwa ikimenyana na Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa Uwanja wa Old Trafford.

Unatajwa kuwa moja ya mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na pia unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka pointi tatu muhimu.

Guardiola amesema:”Huu ni mchezo muhimu zaidi kwetu hii ni dabi ni lazima tujiandae vizuri sana kama tunataka ushindi kwenye mchezo huu kwa kuwa United kwa sasa ina wachezaji bora,” amesema.