
CHAMA AKUBALI KUREJEA SIMBA
ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, amebainisha kwamba, yupo tayari kurudi katika kikosi hicho endapo atatakiwa kufanya hivyo.Chama aliyecheza Simba kwa misimu mitatu kuanzia 2018 hadi 2021, msimu huu amejiunga na RS Berkane ya Morocco. Akiwa Simba, kiungo huyo alipata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 na kiungo bora 2020/21. Simba msimu huu imeanza kwa kasi ya kawaida huku kati ya upungufu ambao umekuwa ukibainishwa ni kukosekana kwa Chama na Luis Miquissone ambao waliondoka mwishoni mwa msimu uliopita. Akizungumzia uwezekano wa kurudi Simba, Chama…