
YANGA YAINGILIA DILI LA BEKI SIMBA
IMEFICHUKA kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga umeingilia dili la kumnasa nahodha wa Biashara United, Abulmajid Mangalo ambaye amekuwa akiwindwa kwa ukaribu na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba. Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, aliwasilisha ripoti ya usajili ambapo miongoni mwa maeneo ambayo amehitaji yafanyiwe maboreshio ni nafasi ya mlinzi wa kati akitaka beki kuja kuwapa changamoto, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto. Mpaka sasa Mangalo amebakisha…