
NYOTA HAWA WAPYA WAIPA KIBURI YANGA
NYOTA wapya wa timu ya Yanga ambao wametua ndani ya dirisha dogo, wameipa jeuri timu hiyo kiasi cha kutamka kuwa wana uhakika wa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi. Mabosi hao wameongeza kuwa wana uhakika huo kwa mastaa hao wapya ndani ya kikosi hicho, wakiamini wana uwezo mkubwa. Miongoni mwa mastaa wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ni Dennis Nkane aliyetoka Biashara United, Aboutwalib Mshery, Salim Aboubakhari ‘Sure Boy’ na Crispin Ngushi. Yanga ni mabingwa watetezi na mchezo wa kwanza mbele ya…