Home Sports NYOTA HAWA WAPYA WAIPA KIBURI YANGA

NYOTA HAWA WAPYA WAIPA KIBURI YANGA

NYOTA wapya wa timu ya Yanga ambao wametua ndani ya dirisha dogo, wameipa jeuri timu hiyo kiasi cha kutamka kuwa wana uhakika wa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi.

Mabosi hao wameongeza kuwa wana uhakika huo kwa mastaa hao wapya ndani ya kikosi hicho, wakiamini wana uwezo mkubwa.

Miongoni mwa mastaa wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ni Dennis Nkane aliyetoka Biashara United, Aboutwalib Mshery, Salim Aboubakhari ‘Sure Boy’ na Crispin Ngushi.

Yanga ni mabingwa watetezi na mchezo wa kwanza mbele ya Taifa Jang’ombe walishinda kwa mabao 2-0 na ule wa pili walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 dhidi ya KMKM.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji walionao ni wazuri, jambo ambalo linawapa imani ya kuweza kutwaa taji la Mapinduzi.

“Sisi ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na tunaweka wazi kwamba dhamira yetu ipo wazi kwamba tunahitaji kulitwaa taji hili na inawezekana hasa ukizingatia kila mchezaji ana uwezo mkubwa na anahitaji kufanya jambo.

“Uwepo wao wa wachezaji wapya pamoja na wale wengine ambao wapo kwa muda inatosha kusema kwamba nini ambacho tunahitaji kukifanya, kilichobaki ni suala la kusubiri na kuona,” amesema Bumbuli.

Yanga imetinga hatua ya nusu fainali na inatarajiwa kumenyana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali unaoatarajiwa kuchezwa kesho Junuari 10.

Previous articleVIDEO:AZAM FC:YANGA WAMEJILETA,BUMBULI ANYAMAZE
Next articleRALF AKIRI NYOTA MAN U WANATAKA KUSEPA