Home Sports SIMBA YAGAWANA POINTI NA MLANDEGE

SIMBA YAGAWANA POINTI NA MLANDEGE

SIMBA leo Januari 7,2022 imetoshana nguvu bila kufungana na Mlandege FC kwenye mchezo wa pili wa Kombe la Mapinduzi.

Dakika 90 zimekamilika kwa ubao wa Uwanja wa Amaan kusoma Simba 0-0 Mlandenge FC.

Licha ya Simba kuanza na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na kipa namba moja Aishi Manula, mshambuliaji wao kibu Dennis pamoja na kiungo Pape Sakho ngoma ilikuwa ni nzito kwao.

Licha yakugawana pointi mojamoja wanafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuwa wana jumla ya pointi nne kibindoni na mabao yao ni mawili.

Mchezo wao ujao wa nusu fainali unatarajiwa kuchezwa dhidi ya Namungo FC.

Previous articleMILANGO MIGUMU DAKIKA 45,SIMBA 0-0 MLANDEGE FC
Next articleUKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI