Home Sports FT:YANGA 2-2 KMKM,YANGA HAO NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

FT:YANGA 2-2 KMKM,YANGA HAO NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

DAKIKA 90 zimekamilika kwa Yanga kugawana pointi mojamoja na KMKM katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan.

Mabao ya Heritier Makambo dakika ya 45 na liliwafanya waweze kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.

Bao la KMKM la ufunguzi lilikuwa ni kupitia kwa Abdlahaman Ali ilikuwa ni dakika ya 55.

Feisal Salum alipachika bao dakika ya 81 na kuwafanya Yanga waamini kwamba wamemaliza kazi ila mambo yakawa tofauti.

Kabla ya mchezo kuisha KMKM walipachika bao la kushtukiza dakika za lala salama na kufanya ubao kusoma Yanga 2-2 KMKM ilikuwa ni dakika ya 90.

Previous articleDAKIKA 45, YANGA 1-0 KMKM
Next articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA MLANDEGE FC NI FULL MKOKO