Home Sports YANGA WAPANIA KUVUNJA REKODI KWA SIMBA

YANGA WAPANIA KUVUNJA REKODI KWA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Morinyo’ ameweka wazi kuwa anataka kufuta uteja mbele ya Simba Queens kwa kushinda kwenye mechi yao ya dabi itakayopigwa leo Jumamosi Januari 8 2022 katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kocha huyo alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano kati ya timu hizo na Waandishi wa Habari uliofanyika jana Ijumaa katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Edna amesema: “Sina matokeo mazuri au Yanga Princess haina matokeo mazuri mbele ya Simba, ila huu ni mchezo na matokeo ni baada ya dakika 90, tumejiandaa kushindana na kushinda.”

Kwa upande wake nahodha wa Yanga Princess, Fatuma Mwisendi, amesema: “Tutahakikisha tunapambana, tutaonyesha mchezo mzuri na wa kiungwana ukizingatia kuwa kikosi chetu kina wachezaji wazoefu, wengi wao wameshacheza dabi tofautinchini kwao, kwa hiyo sidhani kama mchezo wa kesho (leo) utatuzuia sisi kupata ushindi.”

Nahodha wa Simba,Violeth Nicholas, amesema:“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu, muhimu ni kuboresha muendelezo mzuri tulionao kwenye ligi na kushinda mechi zetu na kubakia nafasi ya kwanza kwenye msimamo.”

Previous articleBURUDANI YA SOKA INAHAMIA AFRIKA, AFCON 2022 KIMEUMANA!!
Next articleNI YANGA V AZAM, SIMBA V NAMUNGO, KOMBE LA MAPINDUZI