SIMBA WAVAMIA VYUMBA VYA WACHEZAJI
MARA baada ya kipyenga cha mwisho cha kumaliza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union uliochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, baadhi ya viongozi wa Simba walivamia vyumbani na kufanya kikao kizito na wachezaji wao. Mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu, matokeo hayo hayakuwafurahisha mashabiki, wachezaji, wala viongozi hao, jambo lililolazimika kikao kizito kufanyika fasta.Hiyo ni suluhu ya pili kwa Simba msimu huu ndani ya Ligi Kuu…