CHIKO USHINDI AMPA KIBURI NABI, USHINDANI WA NAMBA NI BALAA!

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa ujio wa kiungo mshambuliaji,Mkongomani, Chico Ushindi, umeongeza ubora na ushindani wa namba katika kikosi chake. Kauli hiyo aliitoa siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania uliotarajiwa kupigwa jana saakumi kamili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Kabla…

Read More

SABABU YA MUKOKO KUSEPA YANGA HII HAPA

RASMI uongozi wa Yanga umethibitisha kwamba kiungo Tonombe Mukoko hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22 kwenye mechi ambazo zimebaki. Kiungo huyo anakwenda kujiunga na kikosi cha TP Mazembe kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi ya mpira ambayo ameichagua. Sababu kubwa ya kiungo huyo kuondoka ni makubaliano ya pande zote mbili kati ya…

Read More

NIGERIA YATOLEWA AFCON

TIMU ya taifa ya Tunisia Carthage Eagles imefanikiwa kuwa timu ya pili kukata tiketi ya kuingia katika robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, (Afcon 2021) baada ya kuibwaga Nigeria-Super Eagles kwa bao 1-0 katika uwanja wa Roumde Adjia mjini Garoua. Tunisia waliandika bao lao la kwanza na la ushindi kupitia kwa mchezaji Youssef Msakni anayechezea klabu ya…

Read More

SIMBA WAAMBULIA POINTI MOJA DAKIKA 180

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa sasa wanapita katika kipindi kigumu kutokana na kuwa kwenye mwendo wa kuchechemea katika vita ya kusaka pointi tatu. Ndani ya Januari kwenye mechi za ugenini wamekwama kusepa na ushindi zaidi ya kuambulia sare moja na kichapo kimoja. Mechi mbili ambazo ni dakika 180 walikuwa kwenye msako wa…

Read More

YANGA WAREJEA DAR NA POINTI ZA KUTOSHA

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamerejea salama Dar baada ya kutoka kusaka pointi sita ugenini. Walianza mbele ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani  Tanga na ubao ukasoma Coastal Union 0-2 Yanga. Mabao ya Fiston Mayele na Said Ntibanzokiza yalitosha kuipa pointi tatu mazima Yanga. Kituo kilichofuata ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, Januari…

Read More

SIMBA YACHEZA DAKIKA 180 BILA KUFUNGA

PABLO Franco ana kazi kubwa ya kufanya kwa sasa ndani ya Simba hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo imeweza kuyeyusha dakika 180  bila kufunga. Ile safu yenye mshambuliaji bora msimu wa 2020/22 John Bocco ambaye alifunga mabao 16 na pasi mbili mpaka sasa bado inapitia wakati mgumu. Ilianza kunyooshwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City…

Read More

KMC YACHEKELEA POINTI NNE UGENINI

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa pointi nne ambazo wamezipata ugenini zitawaongezea nguvu katika kurudi kwenye ubora wao. Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa baada ya kukamilisha safari ya kusaka pointi sita na kupata nne ni hatua kubwa katika harakati za kurejea kwenye ubora. “Tumetoka Dar tukaenda Sumbawanga, (Prisons 0-2 KMC) tukachukua pointi…

Read More

TFF YAFUNGUKIA ISHU YA BOSI SIMBA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeweka wazi kwamba halijamfungulia kesi, Polisi kiongozi yoyote wa mpira wa miguu. Ilikuwa inaelezwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez amefunguliwa mashataka Polisi na kiongozi mmoja wa TFF. Mashtaka hayo ilielezwa kuwa yamefunguliwa katika kituo Kikuu Cha Polisi, Dar, Januari 20,2022 ambapo Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo…

Read More

YANGA YAFUNGUKIA ISHU YA DJUMA SHABAN

BAADA ya jana Januari 23 Yanga kuweza kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania,Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amefungukia kuhusu sakata la beki wao Djuma Shaban kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Djuma dakika ya 89 alionekana akimchezea faulo mchezaji wa Polisi…

Read More

TANZANITE YAITULIZA ETHIOPIA KOMBE LA DUNIA

TIMU ya taifa ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20, ‘Tanzanite’ jana iliweza kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar na ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo. Dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote…

Read More

NAMUNGO YAWABAMIZA 3-1 COASTAL NYUMBANI

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union wamekwama kutamba wakiwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani baada ya kuruhusu kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC, Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Coastal Union waliweza kupewa adhabu hiyo kutokana na makosa ya safu ya ulinzi ambayo ilikwama kuwa makini. Bao la ufunguzi lilifungwa na Obrey Chirwa ambaye…

Read More

YANGA WAITUNGUA POLISI TANZANIA

DICKSON Ambundo kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amefunga bao la 23 ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi. Ni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo aliweza kupachika bao hilo dakika ya 64 kwa pasi ya Fiston Mayele mbele ya Polisi Tanzania. Yanga wanasepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania…

Read More

POLISI TANZANIA 0-0 YANGA

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania ambao nao pia wanahitaji ushindi. Dakika 45 za kipindi cha awali zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid unasoma Polisi Tanzania 0-0 Yanga. Ni mchezaji mmoja anayeitwa Khalid Aucho ameonyeshwa kadi ya njano dakika ya 45 baada…

Read More

CHIKO AKABIDHIWA MAJUKUMU YA JESUS MOLOKO ARUSHA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania, amempa Chiko Ushindi majukumu ya Jesus Moloko. Chico anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi cha Yanga kinachotarajia kucheza mchezo huo utakaopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti…

Read More