DICKSON Ambundo kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amefunga bao la 23 ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Ni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo aliweza kupachika bao hilo dakika ya 64 kwa pasi ya Fiston Mayele mbele ya Polisi Tanzania.
Yanga wanasepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania na kuvunja mwiko wa kutoshinda ugenini mbele ya Polisi Tanzania.
Metacha Mnata ametunguliwa bao hilo kipindi cha pili huku kipindi cha kwanza akiwa katika ubora kwa kuzuia mabao katika lango lake.
Yanga inafikisha pointi 35 ikiwa nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo ndani ya ligi huku Polisi Tanzania ikiaki na pointi 18 na zote zimecheza mechi 13.
Ni bao la kwanza kwa Ambundo ambaye aliibuka hapo akitokea Dodoma Jiji.