Home Sports NAMUNGO YAWABAMIZA 3-1 COASTAL NYUMBANI

NAMUNGO YAWABAMIZA 3-1 COASTAL NYUMBANI

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union wamekwama kutamba wakiwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani baada ya kuruhusu kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC,

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Coastal Union waliweza kupewa adhabu hiyo kutokana na makosa ya safu ya ulinzi ambayo ilikwama kuwa makini.

Bao la ufunguzi lilifungwa na Obrey Chirwa ambaye aliweza kumchambua kipa na kuchagua sehemu ya kufunga katika mchezo wa leo ilikuwa dakika ya 38 na mabao mawili yalifungwa na Relliats Lusajo ilikuwa dakika ya 81 na 85.

Sasa Lusajo ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao saba kibindoni huku akifuatiwa na Fiston Mayele mwenye mabao sita na anakipiga ndani ya Yanga.

Bao la kufuta machozi kwa Coastal Union lilifungwa na Abdulmalick Zakaria aliyejifunga dakika ya 46.

Previous articleYANGA WAITUNGUA POLISI TANZANIA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU