>

COMOROS KUVAANA NA CAMEROON YENYE KINARA WA UTUPIAJI

COMOROS leo wana kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa 16 bora wa Afcon 2021 dhidi ya Cameroon mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Pia kuna uwezekano Comoros ikashuka uwanjani bila ya uwepo wa kipa kutokana na makipa wake kusumbuliwa na majeraha na wengine wanasumbuliwa na Covid-19.

Hata kocha wao Amir Amir Abdou naye anaweza asiwe kwenye benchi la ufundi.

Timu hiyo inashiriki Afcon kwa mara ya kwanza wanamenyana na wenyeji Cameroon ambao wapo kwenye ubora wao na wanaye mshambuliaji matata Vincent Aboubakar ambaye ni kinara kwenye chati ya utupiaji na ana mabao matano.

Meneja wa Comors, El Hadad Himidi amesema kuwa wanajaribu kushughulikia tatizo hilo.

“Tunajaribu kushughulikia na tatizo hili kwa ubora mkubwa iwezekanavyo.

“Bila kocha, wachezaji kadhaa muhimu na makipa wawili waliobaki. Hali ni ngumu mno,”.