>

CHIKO AKABIDHIWA MAJUKUMU YA JESUS MOLOKO ARUSHA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania, amempa Chiko Ushindi majukumu ya Jesus Moloko.


Chico anatarajiwa
kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi cha Yanga kinachotarajia kucheza mchezo huo utakaopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Chanzo kutoka ndani
ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra, kuwa: “Chico amesajiliwa kwenye kikosi cha Yanga kutokana na kuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili jambo ambalo ni nadra kwa wachezaji wengi wanaocheza nafasi ya winga.

 

“Kwa sasa Kocha amekuwa haridhishwi na kiwango cha Moloko kwani alisajiliwa kuwa mbadala wa Tuisila Kisinda, lakini aina ya uchezaji wake sio kama ule aliotarajiwa licha ya kufunga mabao na kutoa asisti.


“Tuisila alikuwa akipata
mipira anakimbia kuingia ndani ya boksi tofauti na Moloko, ukimwangalia Chico
katika mchezo wa kirafiki
dhidi ya Mbuni FC alikuwa akipata mipira anaingia ndani ya boksi mpaka akasababisha
penalti.


“Huenda Chico akachukua
nafasi ya Moloko kwa sababu kocha amefurahishwa na kiwango chake kwani anapopata mpira anatengeneza nafasi tofauti na Moloko ambaye anarudisha mipira nyuma na kuifanya timu kupunguza kasi ya
kushambulia.”