
SALAH AINGIA ANGA ZA BARCELONA
IMEELEZWA kuwa Barcelona imewasiliana na Mohamed Salah ili waweze kupata saini yake ndani ya kikosi hicho. Mshambuliaji huyo raia wa Misri amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake ndani ya Liverpool inayotumia Uwanja wa Anfield. Taarifa ya Daily Mirror inasema kuwa Barcelona ni kama wamemteka akili baada ya kumwambia kwamba wanahitaji awe ndani ya familia yao….