Home Sports MRITHI WA PABLO APEWA MASHARTI MAZITO

MRITHI WA PABLO APEWA MASHARTI MAZITO

IKIWA kwa sasa Simba wanasaka nafasi ya mrithi wa Pablo Franco aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, mabosi wa timu hiyo wamebainisha kwamba kocha ajaye lazima awe na ubora na akubali kufanya vizuri kimataifa.

Pablo alifutwa kazi Simba Mei 31, mwaka huu na mafanikio yake makubwa ilikuwa ni kutwaa Kombe la Mapinduzi na kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku kwenye ligi akiacha timu nafasi ya pili ikikusanya pointi 51.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema mpango uliopo kwa sasa ni kumpata kocha mpya mapema ili afanye usajili kwa kushirikiana na viongozi.

“Kocha mpya ajaye lazima awe na CV kubwa na uzoefu ili atakapopewa projekti ya kuifundisha timu lazima akubali kuweza kwenda sawa na kile ambacho tunakihitaji, kombe la ligi, Kombe la Shirikisho na kuvuka hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tumeishia mara tatu kwenye robo fainali, sasa mawazo yetu ni kuona tunaondoka hapo, mapema kabla ya maandalizi ya msimu mpya hayajaanza kocha atakuwa ameshatambulishwa na kuanza kazi,” alisema Try Again.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
Next articleSALAH AINGIA ANGA ZA BARCELONA