Home Sports YANGA HESABU ZAO ZIPO HIVI

YANGA HESABU ZAO ZIPO HIVI

BAKARI Mwamnyeto nahodha wa Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho wanakihitaji kwenye mechi ambazo wanacheza ni pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa wakiwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Mei 5 2024 walikomba pointi tatu mazima.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Yanga na bao la ushindi likifungwa na Joseph Guede ilikuwa dakika ya 41 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Nahodha huyo amesema wanatambua ushindani uliopo na kikubwa ni kupambana kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi wanazocheza.

“Kikubwa ni alama tatu kwenye mechi ambazo tunacheza tunatambua ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi tunapambana kupata matokeo mazuri.”

Yanga kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 65 baada ya kucheza jumla ya mechi 25 msimu wa 2023/24.

Previous articleLIVERPOOL WAFUFUA MATUMAINI YAO YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND
Next articleSIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA TABORA UNITED