SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA TABORA UNITED

BAADA ya kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, hesabu za Simba ni kupata ushindi mbele ya Tabora United.

Ikumbukwe kwamba Simba ilipata ushindi huo kwenye mchezo wa ligi baada ya kupukutisha siku 50 bila kuambulia ushindi kwenye mechi za ligi.

Ngoma ilikuwa Simba 2-0 Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mei 6 2024 Simba inakibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United ikiwa ni mzunguko wa pili.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo dhidi ya Tabora United wamefanya maandalizi mazuri kupata matokeo chanya.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa ni moja ya timu zenye ushindani lakini tupo tayari kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja hilo linawezekana.

“Kikubwa ambacho kipo kwa wachezaji ni kutumia mchezo huo kufanya vizuri na makosa ambayo yalipita kwenye mchezo wetu tunayafanyia kazi yale mazuri tunayaendeleza.”

Katika mchezo uliopita mabao ya Simba yalifungwa na Michael Fred na mwamba Saleh Karabaka ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo.