Home Sports AZAM FC WANA JAMBO LAO MANUNGU

AZAM FC WANA JAMBO LAO MANUNGU

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wana jambo lao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Ni Morogoro mji kasoro bahari mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili kwa wababe hao unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu.

Miongoni mwa wachezaji ambao wataanza kikosi cha kwanza ni pamoja na Lusajo Mwaikenda, Yahya Zayd, Sopu, Lyanga na Fei Toto ikiwa kamili kuwakabili Mtibwa.

Ikumbukwe kwamba Azam FC ni namba mbili kwenye msimamo wa ligi mchezo wao ujao ni Mei 9 itakuwa Mzizima Dabi dhidi ya Simba iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Vinara ni Yanga ambao baada ya kucheza mechi 25 wamekomba pointi 65 kibindoni.

Yusuph Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa vijana wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar malengo ni kupata pointi tatu.

“Kila timu ambayo tunakutana nayo ni ngumu na kikubwa ni kuona tunapata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza,”.

Previous articleAZIZ KI NA GUEDE NI HABARI NYINGINE HUKO YANGA/UBINGWA WANUKIA
Next articleMTIBWA SUGAR 0-2 AZAM FC