Home Sports HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA

HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA

LIGI Kuu Tanzania Bara  inazidi kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa pili ambapo timu zinaendelea kupambania pointi tatu.

Ipo wazi kwamba vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga ilisepa na pointi tatu kwenye mchezo wake Mei 5 2024 ubao uliposoma Mashujaa 0-1 Yanga bao likifungwa na Joseph Guede dakika ya 41 sasa inafikisha pointi 65.

Mei 6 2024 Simba inayonolewa na Juma Mgunda itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Azam Complex.

Matajiri wa Dar, Azam FC wapo Morogoro, mji kasoro bahari watakuwa Uwanja  wa Manungu kuwavaa Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Coastal Union itakuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuwakaribisha Tanzania Prisons.

Previous articleShindano la Expanse Kasino Maokoto Kama Yote. Cheza kwa Kuanzia Tsh 400/=
Next articleSTAMINA AFICHUA KILICHOMUUA DIRECTOR KHALFANI…