Home Entertainment STAMINA AFICHUA KILICHOMUUA DIRECTOR KHALFANI…

STAMINA AFICHUA KILICHOMUUA DIRECTOR KHALFANI…

Staa wa Bongo Fleva, Stamina ‘Shorobwenzi’ amesema kifo cha Dairekta Khalfani ni pigo kubwa kwa sanaa ya muziki wa kizazi kipya kwani alikuwa ni mtu wa kutegemewa linapokuja suala la kushoot video za nyimbo za wasanii.

Amesema kwa taarifa ambazo alikuwa anazijua, ni kwamba Dairekta Khalfan alianguka akiwa kazini na baadaye akapelekwa Hospitali ya Lugalo kabla ya kuhamishiwa Muhimbili (MOI) na kusisitiza kwamba yeye siyo msemaji bali familia ndiyo inayoweza kueleza ni nini hasa kilichotokea.

Dairekta Khalfan amezikwa leo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, huku wasanii wengi wakihudhuria mazishi hayo.

Previous articleHII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA
Next articleAMEWEKWA MTU KATI MWAMBA CHAMA