IMEELEZWA kuwa Barcelona imewasiliana na Mohamed Salah ili waweze kupata saini yake ndani ya kikosi hicho.
Mshambuliaji huyo raia wa Misri amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake ndani ya Liverpool inayotumia Uwanja wa Anfield.
Taarifa ya Daily Mirror inasema kuwa Barcelona ni kama wamemteka akili baada ya kumwambia kwamba wanahitaji awe ndani ya familia yao.
Kwa mujibu wa Mirror, Salah ameahidiwa usajili huru kwenda hapo Nou Camp kipindi cha usajili kijacho cha majira ya joto.
Salah amekuwa chachu kubwa ya mafanikio ndani ya Liverpool tangu ajiunge hapo mwaka 2017 akitokea Roma kwa dau la pauni milioni 37.
Amefunga mabao 156 na kutoa pasi za mabao 63 katika mechi 254 za michuano yote.