Home Uncategorized MIPANGO MIKUBWA YA USAJILI YANGA NI KIMATAIFA

MIPANGO MIKUBWA YA USAJILI YANGA NI KIMATAIFA

 UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umeweka wazi kuwa msimu ujao malengo yao ni kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa wanayotarajia kushiriki kutokana na kuwa kwenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22.

Yanga inahitaji pointi tatu ili kutwaa ubingwa wa ligi pia imetinga Fainali ya Kombe la FA kwa kuwaondoa watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Hersi Said amesema moja ya mikakati yao ni kuzidi kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na uzoefu.

“Tunataka kufanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao kwa haya ambayo yametokea msimu huu bado hayajawa makubwa ni suala la mashabiki kuweza kuwa na subira.

“Mafanikio ambayo tunayataka ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote na hapa wachezaji wengi wanapenda kuja kucheza kutokana na ubora ambao tupo nao,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kusajiliwa na Yanga ni kiungo wao wa zamani Bernard Morrison ambaye alikuwa akicheza Simba na mkataba wake unaisha msimu huu wa 2021/22.

Previous articleNAMNA YA KUCHEZA, NA KUSHINDA KENO MERIDIANBET!
Next articlePOGBA KUVUTA MKWANJA MREFU UNITED