Home Sports POGBA KUVUTA MKWANJA MREFU UNITED

POGBA KUVUTA MKWANJA MREFU UNITED

IMEFICHUKA kuwa Paul Pogba ataondoka na bonasi ya pauni milioni 3.78 (Sh bilioni 11) atakapoachana na Manchester United mara baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa mwezi huu.

United ilithibitisha kuwa kiungo huyo Mfaransa ataondoka Old Trafford mkataba wake utakapomalizika Juni 30, huku pia ikithibitishwa kuwa Jese Lingard naye anasepa.

Licha ya kuwa na kiwango duni na majeraha ya mara kwa mara katika misimu yake miwili ya mwisho, Pogba atapewa posho ya utumishi, pauni milioni 3.78, kama walivyokubaliana kwenye mkataba.

Hiyo siyo habari itakayopokelewa vizuri na mashabiki wa Man United ambao hawajaona ubora wa mshindi huyo wa Kombe la Dunia tangu arejee kwa mara ya pili Old Trafford akiwa amecheza kwa miaka sita hadi sasa.

Nyota huyu rasmi amekuwa hasara kwa United ambayo ilimlipa dau la usajili wa rekodi ya dunia, pauni 89m, alipokuwa akirejea kutokea Juventus mwaka 2016, baada ya kumpoteza kwa Waitaliano hao kwa kulipwa fidia ya pauni 1.5m tu mwaka 2012.

Licha ya kulipa kitita hicho kikubwa, United pia ilimlipa wakala wa mchezaji huyo, marehemu Mino Raiola pauni 39.27m (Sh bilioni 114).

Pogba pia alikuwa akilipwa kwa mwaka mshahara wa pauni 7.75m (Sh bilioni 22.5), malipo ya haki za matangazo pauni 2.87m (Sh bilioni 8.4) na posho ya pauni 1.875m (Sh bilioni 5.4) katika kila msimu, kwa misimu minne ambayo United ilifuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Licha ya kuwekeza fedha zote hizo, United haitaambulia chochote kwa Pogba, kwa kuwa anaondoka bure.

Previous articleMIPANGO MIKUBWA YA USAJILI YANGA NI KIMATAIFA
Next articleJIMMY KINDOKI: ENG.HERSI ANAFAHA KUWA RAIS WA YANGA – VIDEO