Home Sports JUVENTUS YAMVUTIA KASI POGBA

JUVENTUS YAMVUTIA KASI POGBA

KIUNGO mshambuliaji wa Manchester UnitedPaul Pogba inatajwa kwamba anaweza kujiunga na Juventus ambayo imemuwekea mkwanja mrefu kupata saini yake.

Nyota huyo mkataba wake unatarajiwa kumeguka ndani ya Manchester United mwisho wa msimu huu na hana mpango wa kuongeza dili jipya kwa kuwa tayari ameshawaaga maosi wake.

Alijiunga na United akitokea Klabu ya Juventus na ametoa huduma kwenye kikosi hicho kwa muda wa miaka 6.

Taarifa zinaripoti kwamba Rafaela Pimentala mwanasheria na wakala wa Pogba ambaye amechukua nafasi ya Mino Raiola ambaye amefariki atakuwa jijini Turin kukamilisha dili hilo.

Previous articleSIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMCHIMBISHA PABLO
Next articleANTONIO RUDIGER ASANI MIAKA MINNE REAL MADRID