Home Sports SIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMCHIMBISHA PABLO

SIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMCHIMBISHA PABLO

MABOSI Simba  wameweka wazi kwamba kushindwa kutimiza yale aliyosaini kwenye mkataba ni sababu iliyofanya kufutwa kazi kwa Pablo Franco aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba.

Mei 31,Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez waliweka wazi kwamba wamefikia makubaliano ya kuachana na Pablo kwenye nafasi hiyo na timu kwa sasa ipo chini ya Seleman Matola ambaye ni Kocha Msaidizi.

Salim Abdallah, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba amesema kuwa mkataba wa Simba na makocha ni mradi ambao unakuwa na maelekezo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi na kila anayekubali kusaini.

“Mkataba wetu na makocha ni project, (mradi) hivyo unaona kwamba hata Pablo, (Franco) yeye alisaini na kulikuwa na makubaliano kwamba achukue ubingwa wa ligi,Kombe la Shirikisho na kufika hatua ya nusu fainali kimataifa na mwisho wa siku hakufanikiwa, unadhani nini kitatokea.

“Tunajua kwamba ni kocha mzuri alikuwa na CV nzuri lakini hakuwa na uzoefu na soka la Afika tumeachana naye kiroho safi na sisi sio wachawi tunajua kwamba amepata dili sehemu nyingine tunamtakia kila la kheri.

“Ilikuwa hivyo hata kwa mtangulizi wake Da Rosa, (Didier) huyu tuliletewa barua kwamba hajakidhi vigezo na ndio maana kuna mechi alikuwa anaongoza akiwa jukwaani, lakini mechi za mwanzo za ligi alianza kwa tabu na tulitolewa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo tuliachana naye kwa amani,”.

Previous articleKAMBOLE AINGIA ANGA ZA YANGA
Next articleJUVENTUS YAMVUTIA KASI POGBA