Home Sports KAMBOLE AINGIA ANGA ZA YANGA

KAMBOLE AINGIA ANGA ZA YANGA

 IMEELEZWA kuwa Lazarous Kambole anayekipiga ndani ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini yupo kwenye hesabu za  mabosi wa Yanga.

Huyo ni mshambuliaji wa kimataifa ambaye anatajwa kuwa kwenye hesabu za vinara hao wa ligi ambao wapo kwenye kusubiri hesabu zikamilike watwae taji la Ligi Kuu Bara kwa kuwa wamewaacha wapinzani wao Simba kwa jumla ya pointi 13.

Jambo la kuisaka saini ya nyota huyo ni kuimarisha kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia.

Nyota huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo msimu utakapomeguka hivyo atakuwa huru kujiunga na timu hiyo bure ikiwa hataongezewa mkataba wake.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga,Injinia Hersi Said amesema kuwa usajili ni siri hivyo mambo yote ambayo watafanya ni kwa mpango kazi maalumu.

“Usajili ni siri ya klabu hivyo hivi sasa tutafanya mambo yote kwa siri na usajili ambao tutafanya tuna amini kwamba utakuwa mzuri,” amesema.

Previous articleSHIME:CAMEROON WAGUMU,LAKINI TUTASHINDA
Next articleSIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMCHIMBISHA PABLO