Home Sports SHIME:CAMEROON WAGUMU,LAKINI TUTASHINDA

SHIME:CAMEROON WAGUMU,LAKINI TUTASHINDA

 BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa za Wanawake Tanzania,amesema kuwa mchezo wa marudiano baina yao dhidi ya Timu ya Taifa ya Wasichana wa U 17 Serengeti Girls dhidi ya Cameroon kuwania Kufuzu Kombe la Dunia hautakuwa rahisi.

Licha ya kutambua kwamba mchezo huo hautakuwa rahisi kutokana na kila timu kuhitaji ushindi, Shime amebainisha kwamba watakwenda kufanya vizuri na kupata ushindi.

Mchezo huo ni wa marudio unatarajiwa kuchezwa kesho Jumapili, Zanzibar na Cameroon watakuja na nguvu ya kutafuta ushindi baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 wakiwa Cameroon.

“Mchezo ni mgumu sana haitakuwa jambo rahisi kucheza dhidi ya Cameroon tena wao watakuja kwa lengo la kutaka kuvuka wakiwa ugenini na sisi tunahitaji kusonga mbele,”.

Serengeti Girls wakivuka hapo kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar,watakuwa wamekata tiketi ya kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika India Oktoba mwaka huu

Previous articleMWENDO WA BIASHARA UNITED NA MBEYA KWANZA UNA JAMBO LAO
Next articleKAMBOLE AINGIA ANGA ZA YANGA