Home Sports SIMBA:TUTASAJILI WACHEZAJI WENYE NJAA YA MAFANIKIO

SIMBA:TUTASAJILI WACHEZAJI WENYE NJAA YA MAFANIKIO

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba,Salim Abdallah amesema kuwa msimu ujao watafanya usajili mkubwa kwa kuleta wachezaji wenye njaa ya mafanikio.

Kwa sasa Simba ipo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya baada ya Mei 31,2022 kumchimbisha Pablo Franco ambeya alikuwa kwenye benchi la ufundi.

Mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa Mei 28 mbele ya Yanga na kuwafanya waweze kuondolewa kwenye hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho.

Abdallah amesema:”Tutafanya usajili wa wachezaji wenye njaa ya mafanikio na kuna wachezaji kadhaa ambao wataweza kuachwa kwa kuwa wapo ambao mikataba yao inaisha,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kufika tamati ni Pascal Wawa,Joash Onyango.

Previous articleANTONIO RUDIGER ASANI MIAKA MINNE REAL MADRID
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI