Home Sports STARS YAREJEA KUANZA KUIPIGIA HESABU ALGERIA

STARS YAREJEA KUANZA KUIPIGIA HESABU ALGERIA

BAADA ya kupata pointi moja ugenini Jana Juni 4,2022 leo Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, imewasili Dar kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere wakitokea Cotonou, Benin walipokuwa kwenye mchezo wa Kundi F kufuzu AFCON.

Kwenye mchezo huo dhidi ya Niger ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuwafanya Stars kupata pointi moja.

Bao la Stars lilipachikwa dk ya 1 kupitia kwa mshambuliaji George Mpole baada ya kipa wa Niger kutema mpira uliopigwa na Simon Msuva.

 Taifa Stars inaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa pili dhidi ya Algeria utakaochezwa Juni 8, 2022 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
Next articleVIJANA REAL MARDRID WAFICHUA SIRI ZA UBINGWA