
WACHEZAJI WALIOONGEZWA STARS WAONGEZA NGUVU
HEMED Morocco, kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kuongezeka kwa wachezaji katika kikosi hicho kunaongeza upana wa kuchagua kikosi kitakachoanza dhidi ya Uganda. Ni Mohamed Hussein na Shomari Kapombe hawa wameongezwa katika timu ya Tanzania inayofanya maandalizi ya mwisho kuikabili Uganda. Ni kesho Uwanja wa Mkapa saa 2:00 usiku…